19 Mei 2016 - 20:52
Mashambulizi makali ya kuikomboa Fallujah yaanza

Mkuu wa kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu cha Nujabaa nchini Iraq ametangaza kukaribia kuanza kwa mashambulizi makali ya kuikomboa wilaya ya Fallujah nchini Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kiongozi mkuu wa kikundi cha wapiganaji wa kiislamu wa Nujabaa katiika mazungumzo yake ameashiria kuwa tayari maandalizi ya mashambulio makali ya kuikomboa wilaya Fallujayako tayari huku akisisitia kuwa: wapiganaji wa kikundi cha Nujabaa wakishirikiana na kikosi cha kuukomboa mkoa wa Anbar, ambao asilimia kubwa ya wapiganaji wake ni wakazi wa wilaya ya Alkarmah na Falluja wako tayari kimashambulizi, kwa maana siku ya Jumanne iliopita walishakusanyika kutoka maeneo mbalimbali kwajili ya kushiriki katika mashambulizi hayo.
Sheikh “Akram Al Kaabiy” amesema kuwa wilaya ya Falluja ndio makao makuu ya magaidi wa Daesh nchini Iraq, na kusisitiza kuwa mashambulizi hayo yatasambaratisha magaidi hao wilayani humo na kusafishwa wilaya hiyo kutokana na magaidi wa Daesh.
Aidha ameongeza kusema kuwa mashambulizi ya kuikomboa Fallujah ni moja ya hatua ya kulipa kisasi cha damu za mashahidi walio uwawa wilayani hum kupitia magaidi wa Daesh, nasi tunaambatana na kuahidi kwa wananchi wa Iraq kuwa bilashaka tutaakisha tulipiza damu za mashaidi na kuwasambaratisha magaidi katika ardhi ya Iraq.
Kiongozi huyo wa kikundi cha wapiganiji wa kiislamu wa Nujabaa nchini Iraq amewataka wanachi kuwaombea kwa mwenyezi mungu ili wapate ushindi dhidi ya magaidi hao, huku akisisitizia wananchi wa Iraq kuwa ushindi unakaribia.  
mwisho wa Habari/290